Yobu 3
3
Yobu anaomboleza
1Kisha hayo, Yobu akaamua kusema. Akalaani siku aliyozaliwa. #Ang. Yer 20.14-18 2Yobu akasema:
3Iangamie siku ile niliyozaliwa,
usiku ule iliposemwa: “Mimba ya mutoto mwanaume imepatikana.”
4Siku ile ikuwe giza!
Na kutoka juu Mungu asijishugulishe nayo,
wala mwangaza wowote usiiangaze!
5Itawaliwe na giza kubwa sana,
mawingu mazito yaifunike.
Giza la muchana liitishe!
6Usiku ule giza kubwa liufunike!
Usihesabiwe katika siku za mwaka,
usitiwe katika hesabu ya siku za mwezi.
7Usiku ule ukuwe tasa,
sauti ya furaha isiingie ndani yake.
8Ulaaniwe na wale wanaolaani siku,
wale wafundi wanaoamusha Leviatani.
9Nyota zake za mapambazuko zififie,
utamani kupata mwangaza, lakini usipate,
wala usione mwangaza wa mapambazuko.
10Usiku ule ukuwe hivi, kwa sababu haukufunga tumbo la mama,
wala kuficha taabu nisizione.
11Kwa nini sikukufa nilipozaliwa?
Kwa nini kutoka tu katika tumbo sikutoweka?
12Kwa nini mama yangu alinizaa?
Kwa nini nilipata kunyonya?
13Maana ningekuwa nimezikwa, kimya;
ningelala na kupumzika
14pamoja na wafalme na watawala wa dunia
waliojijengea upya miji kutoka mabomoko,
15pamoja na wakubwa waliokuwa na zahabu,
waliojaza nyumba zao feza tele.
16Kwa nini sikukuwa kama
mutoto aliyezaliwa mufu
ambaye hakuona mwangaza?
17Kule kwa wafu waovu hawasumbui mutu,
kule wanaochoka wanapumzika.
18Kule wafungwa wanastarehe pamoja,
hawasikii hata kidogo sauti ya wasimamizi.
19Wakubwa na wadogo wako kule,
nao watumwa wamepata uhuru mbali na bwana zao.
20Kwa nini kumujalia mwangaza na uzima
yule anayekuwa katika taabu,
anayekuwa na huzuni ndani ya moyo,
21anayetamani kifo lakini hakufi,
anayetafuta kifo kuliko hazina iliyofichwa. #Ang. Ufu 9.6
22Mutu kama yule atashangilia sana na kufurahi
atakapokufa na kuzikwa!
23Kwa nini kumujalia uzima mutu ambaye njia zake zimefungwa,
mutu ambaye Mungu amemwekea kizuizi?
24Kuugua ndicho chakula changu.
Malalamiko yangu yanatiririka kama maji.
25Kile ninachoogopa kimenipata;
ninachohofu ndicho kilitokea.
26Sina amani wala utulivu;
sipumziki, taabu imenifikia.
Currently Selected:
Yobu 3: SWC02
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

:
Highlight
Copy
Compare
Share
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.