Isaya 61:1-3
Isaya 61:1-3 SWC02
Roho wa Bwana wetu Yawe yuko pamoja nami, maana Yawe amenichagua, akanituma niwahubirie wanaoteswa habari njema, niwatunze waliovunjika moyo, niwatangazie waliohamishwa kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa. Amenituma kutangaza mwaka wake wa neema, na siku ya Mungu wetu ya kulipiza kisasi kusudi niwafariji wote wanaoomboleza. na kuwapa wale wanaoomboleza katika Sayuni taji la maua pahali pa majivu juu ya kichwa, mafuta ya kuangarisha kwa furaha pahali pa maombolezo, nguo ya sifa pahali pa moyo muzito. Nao wataitwa miti ya mialo ya haki, Yawe aliyopanda kuonyesha utukufu wake.





