2 Mambo ya Siku 5
5
1Basi, Solomono akamaliza kazi zote zilizoelekea nyumba ya Yawe. Kisha Solomono akaleta mali yote baba yake Daudi aliyokuwa ameitoa kwa Mungu, ni kusema: feza, zahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mungu. #Ang. 2 Sam 8.11; 1 Sik 18.11
Sanduku la Ageno linaletwa ndani ya hekalu
(1 Fal 8.1-9)
2Basi mufalme Solomono akawakusanya kule Yerusalema wazee na viongozi wote wa makabila wa ukoo za Waisraeli kusudi waondoe Sanduku la Agano la Yawe kutoka katika muji wa Daudi, ni kusema Sayuni. #Ang. 2 Sam 6.12-15; 1 Sik 15.25-28 3Halafu wote wakakutana mbele ya mufalme katika sikukuu ya mwezi wa saba. 4Nyuma ya wazee wote wa Waisraeli kufika, Walawi wakabeba Sanduku la Agano, 5Walawi na makuhani wakahamisha Sanduku la Agano na hema la mukutano na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa mule ndani ya hema. 6Mufalme Solomono na mukutano wa Waisraeli wakakusanyika mbele ya Sanduku la Agano nao wakatoa sadaka ya ngombe na kondoo wasiohesabika. 7Kisha makuhani wakaingiza Sanduku la Agano la Yawe pahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, Pahali Patakatifu Sana, chini ya mabawa ya makerubi. 8Wale makerubi walitandaza mabawa yao juu ya pahali palipowekwa sanduku, kwa hiyo sanduku na miti yake ya kulibebea vilikuwa chini ya mabawa. 9Kwa sababu miti ile ilikuwa mirefu sana, incha zake ziliweza kuonekana kutoka Pahali Patakatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutoka upande wa inje. Miti ile ingali pahali pale hata leo.
10Ndani ya Sanduku la Agano, hamukukuwa kitu kingine isipokuwa tu vile vibao viwili ambavyo Musa aliviweka mule kule Horebu, pahali Yawe alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka Misri. #Ang. Kumb 10.5
11Kisha makuhani wakatoka pale Pahali Patakatifu, kwa sababu makuhani wote waliokuwa pale bila kujali makundi yao, walikuwa wamejitakasa. 12Walawi wote waimbaji, pamoja na Asafu, Hemani, na Yedutuni, pamoja na Walawi wengine wa ukoo zao, wakiwa wamevaa nguo zao za kitani safi nao wakabeba matoazi, vinanda na vinubi, walisimama upande wa mashariki wa mazabahu. Makuhani mia moja na makumi mbili wapiga baragumu walikuwa pamoja nao. 13Waimbaji na wapiga baragumu wote pamoja walitoa sauti kwa pamoja na matoazi na vyombo vingine vya muziki, wakimusifu Yawe wakiimba: “Yeye ni muzuri. Wema wake unadumu milele.” Wakati ule nyumba ya Yawe ikajazwa na wingu. #Ang. 1 Sik 16.34; 2 Sik 7.3; Ezra 3.11; Zab 100.5; 106.1; 116.1; 136.1; Yer 33.11 #Ang. Kut 40.34-35 14Nao makuhani walishindwa kutumika kwa sababu ya wingu lile, maana utukufu wa Yawe ulijaza nyumba ya Mungu.
Currently Selected:
2 Mambo ya Siku 5: SWC02
Highlight
Share
Compare
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

: