YouVersion Logo
Search Icon

Tito 1

1
Salamu
1Paulo, mtumwa wa Mungu, na mtume wa Yesu Kristo; kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli ile iletayo utauwa; 2katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele; 3#Efe 1:9,10; 1 Tim 1:1,11 akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliokabidhiwa kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu; 4#2 Kor 8:23; Gal 2:3; 2 Tim 4:10; 1 Tim 1:2 kwa Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.
Tito akiwa Krete
5Kwa sababu hii nilikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuwateua wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; 6#1 Tim 3:2-7 ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. 7#1 Kor 4:1; 1 Pet 5:2; 2 Tim 2:24 Maana imempasa askofu#1:7 Askofu: maana yake ni, Mwangalizi. awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu; 8bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake; 9#Tit 2:1; 1 Tim 1:10; 2 Tim 4:3 akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
10Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. 11#Tit 3:6; Yn 10:12; 1 Pet 5:2 Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu. 12Mmoja wao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi wavivu. 13#2 Tim 4:2 Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani; 14#1 Tim 4:7 wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu waukataao ukweli. 15#Mt 15:11; Rum 14:20 Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia. 16#2 Tim 3:5 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala hawafai kwa tendo lolote jema.

Currently Selected:

Tito 1: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy