YouVersion Logo
Search Icon

Mathayo 1

1
Ukoo wa Yesu Kristo
1 # Lk 3:23-38 #1 Nya 17:11; Mwa 5:1; 22:18 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu.
2 # Mwa 21:3,12; 25:26; 29:35; 49:10; 1 Nya 1:34 Abrahamu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; 3#1 Nya 2:5,9; Mwa 38:29,30; Rut 4:18-22; 1 Nya 2:10-12 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu; 4Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni; 5#Rut 4:13-17 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese; 6#2 Sam 12:24 Yese akamzaa mfalme Daudi.
Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria; 7#1 Nya 3:10-14 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa; 8Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; 9Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia; 10Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia; 11#2 Fal 24:14-15; 2 Nya 36:10; Yer 27:20; 1 Nya 3:15,16 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
12 # 1 Nya 3:17; Ezr 3:2 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; 13Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; 14Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; 15Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; 16#Mt 27:17,22 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
17Basi vizazi vyote tangu Abrahamu hadi Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hadi ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hadi Kristo ni vizazi kumi na vinne.
Kuzaliwa kwa Yesu Kristo
18 # Lk 1:27,35 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20#Mt 1:18 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21#Lk 1:31; 2:21; Mdo 4:12 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao. 22#Isa 7:14 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,
23 # Isa 7:14 Tazama, bikira atachukua mimba,
Naye atazaa mwana;
Nao watamwita jina lake Imanueli;
Yaani, Mungu pamoja nasi.
24Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; 25#Lk 2:21; 2:7 asimjue kamwe hadi alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.

Currently Selected:

Mathayo 1: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy