YouVersion Logo
Search Icon

Oba 1

1
Kiburi cha Edomu Kitashushwa
1 # Isa 21:11; Eze 25:12-14; Yoe 3:19; Mal 1:3 Maono yake Obadia.
Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu;
Tumepata habari kwa BWANA,
Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa,
Akisema, Haya, inukeni ninyi;
Na tuinuke tupigane naye.
2Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa;
Umedharauliwa sana.
3 # 2 Fal 14:7; 2 Nya 25:12; Isa 14:13; Ufu 18:7 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya,
Wewe ukaaye katika pango za majabali,
Mwenye makao yako juu sana;
Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
4 # Ayu 20:6; Isa 14:14,15; Yer 49:16; Amo 9:2; Hab 2:9 Ujapopanda juu kama tai,
Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota,
Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.
Ukatili wa Edomu Walipizwa kwa Uporaji na Mauaji
5Kama wevi wangekujilia, kama wanyang’anyi wangekujilia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujilia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe? 6Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwa-tafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwa-ulizwa!
7Watu wote wa mapatano yako
Wamekufukuza, hata mipakani;
Wale waliofanya amani nawe
Wamekudanganya, na kukushinda;
Walao mkate wako wameweka mtego chini yako;
Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
8Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA. 9#Zab 76:5; Yer 49:22; Amo 2:16; Nah 3:13Na mashujaa wako, Ee Temani, watafadhaika, hata iwe kila mtu akatiliwe mbali kwa kuuawa katika kilima cha Esau.
Edomu Alimdhulumu Nduguye
10 # Mwa 47:21; Zab 137:7; Eze 35:5,15; Amo 1:11; Mal 1:4 Kwa sababu ya udhalimu aliotendwa ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele. 11#Nah 3:10Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao. 12#Mik 4:11; Mit 24:17Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao. 13Usiingie katika lango la watu wangu, siku ya msiba wao; naam, usiyatazame mateso yao, siku ya msiba wao; wala usitie mikono yako juu ya mali zao, siku ya msiba wao. 14#Isa 34:5-17; 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Amo 1:11-12; Mal 1:2-5Wala usisimame penye njia panda, ili kuwakatilia mbali watu wake wakimbiao; wala usiwatoe watu wake waliosalia, katika siku ya dhiki. 15#Amu 1:7; Zab 137:8; Eze 35:15; Yoe 3:7,8Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe. 16Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kubabaika, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.
Ushindi wa Mwisho wa Israeli
17Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao. 18Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo. 19#Sef 2:7Na watu wa Negebu wataumiliki mlima wa Esau; na watu wa Shefela watawamiliki Wafilisti; nao watalimiliki konde la Efraimu, na konde la Samaria, na Benyamini atamiliki Gileadi. 20#1 Fal 17:9Na watu wa jeshi hili la wana wa Israeli waliotekwa, walio kati ya Wakanaani, watamiliki mpaka Sarepta; na hao watu wa Yerusalemu waliotekwa, waliomo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu. 21#Isa 19:20; Dan 2:24; Zek 14:9; Ufu 11:15Tena waokozi watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya BWANA.

Currently Selected:

Oba 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy