YouVersion Logo
Search Icon

Yn 17

17
Yesu Awaombea Wanafunzi wake
1 # Yn 11:14; 13:1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 2#Mt 11:27kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. 3#1 Yoh 5:20; 1 The 1:9Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 4#Yn 4:34Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. 5#Yn 1:1; 17:24; Flp 2:6Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. 6#Yn 17:9; Mt 6:9Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. 7Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. 8#Yn 16:30Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 9#Yn 6:37,44Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; 10#Yn 16:15; Lk 15:31na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao.
11 # Yn 10:30; Mt 6:13 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. 12#Zab 41:9; 109:8; Yn 13:18; 6:39; 2 The 2:3Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. 13#Yn 15:11Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14#Yn 15:19Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15#2 The 3:3; 1 Yoh 5:18; Mt 6:13; Lk 22:32Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 17#Yn 6:63Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 18#Yn 20:21Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. 19#Ebr 10:10Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.
20 # Yn 17:9 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21#Gal 3:28Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22#Mdo 4:32Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23#1 Kor 6:17; Gal 2:20Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24#Yn 10:29; 12:26; Efe 1:4Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. 25Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Currently Selected:

Yn 17: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy