YouVersion Logo
Search Icon

Mt 5

5
Sifa na Heri
1 # Lk 6:20-49 Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; 2akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
3 # Isa 57:15 Heri walio maskini wa roho;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 # Isa 61:2; Zab 126:5; Ufu 7:17 Heri wenye huzuni;
Maana hao watafarijika.
5 # Zab 37:11 Heri wenye upole;
Maana hao watairithi nchi.
6 # Isa 55:1-2 Heri wenye njaa na kiu ya haki;
Maana hao watashibishwa.
7 # Yak 2:13 Heri wenye rehema;
Maana hao watapata rehema.
8 # Zab 24:3-4; 51:10; 73:1; 1 Yoh 3:2,3 Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.
9 # Ebr 12:4 Heri wapatanishi;
Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10 # 1 Pet 3:14 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki;
Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 # 1 Pet 4:14 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12#2 Nya 36:16; Mdo 7:52; Yak 5:10; Ebr 11:33-38Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Chumvi na Nuru
13 # Mk 9:50; Lk 14:34-35 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 # Yn 8:12; 9:5 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 15#Mk 4:21; Lk 8:16; 11:33Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 16#1 Pet 2:12; Efe 5:8,9Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Sheria na Manabii
17 # Mt 3:15; Rum 3:31; 10:4 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18#Lk 16:17; 21:33Kwa maana, amin,#5:18Amin taz. 2 Wakorintho 1:20, Ufunuo 3:14. Maana yake ni Ni hakika, au Ni kweli hasa nisemayo. Hilo ni neno la Kiaramu lisilofasiriwa kwa Kiyunani. Ni neno lililotamkwa, kwa lugha iyo hiyo ya Kiaramu, na Yesu Kristo mwenyewe. Litumiwapo mwisho wa sala, maana yake ni Na iwe hivyo. nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. 19#Yak 2:10; 1 Kor 15:9Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Kuhusu Hasira
21 # Kut 20:13; 21:12; Law 24:17; Kum 5:17; 17:8 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22#1 Yoh 3:15Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. 23#Mk 11:25Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, 24iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. 25#Mt 6:14,15; 18:35; Lk 12:58,59Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. 26Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Kuhusu Uzinzi
27 # Kut 20:14; Kum 5:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28#Ayu 31:1; 2 Pet 2:14lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29#Mt 18:8,9; Mk 9:42,47; Kol 3:5Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 30#Mt 18:8; Mk 9:43Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
Kuhusu Talaka
31 # Kum 24:1-4; Mt 19:7; Mk 10:4 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32#Mt 19:9; Mk 10:11-12; Lk 16:18; 1 Kor 7:10-11lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
Kuhusu Viapo
33 # Law 19:12; Hes 30:2; Kum 23:21; Kut 20:7 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; 34#Yak 5:12; Isa 66:1; Mt 23:16-22; Mdo 7:49lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35#Isa 66:1; Zab 48:2wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37#2 Kor 1:17; Yak 5:12Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
Kuhusu Kujilipiza Kisasi
38 # Kut 21:24; Law 24:20; Kum 19:21 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39#Lk 6:27-36#Yn 18:22,23; Law 19:18Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. 40#1 Kor 6:7Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. 41Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. 42Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
Upendo kwa Adui
43 # Law 19:18 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44#Kut 23:4,5; Rum 12:14,20; Lk 23:34; Mdo 7:59lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 45#Efe 5:1ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48#Law 19:2; Kum 18:13Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Currently Selected:

Mt 5: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy