YouVersion Logo
Search Icon

Lk 10

10
Huduma ya wale Sabini
1 # Mt 10:7-16 # Mk 6:7 Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. 2#Mt 9:37-38; Yn 4:35Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. 3#Mt 10:16Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. 4#Mt 10:7-14; Mk 6:8-11; Lk 9:3-5#2 Fal 4:29; Lk 9:3-5Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. 5Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; 6na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. 7#1 Kor 9:14; 1 Tim 5:18Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. 8#1 Kor 10:27Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; 9waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia. 10#Mdo 13:51Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, 11#Mdo 18:6Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. 12#Mwa 19:24-28; Mt 11:24; 10:15Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.
Huzuni kwa Miji Isiyotubu
13 # Isa 23:1-18; Eze 26:1—28:26; Yoe 3:4-8; Amo 1:9-10; Zek 9:2-4; Mt 11:21-23 Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. 14Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi. 15#Isa 14:13-15Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu. 16#Mt 10:40; Mk 9:37; Lk 9:48; Yn 5:23; 15:23; 13:20Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
Kurudi kwa wale Sabini
17Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18#Yn 12:31; Ufu 12:8,9Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 19#Zab 91:13; Mk 16:18Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. 20#Kut 32:32; Flp 4:3; Ufu 3:5; Mt 7:22Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
Yesu Ashangilia
21 # Mt 11:25-27 Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. 22#Yn 3:35; 10:15Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. 23#Mt 13:16,17Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi. 24#1 Pet 1:10Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.
Mfano wa Msamaria Mwema
25 # Mt 22:35-40; Mk 12:28-34 # Lk 18:18-20 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? 26Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? 27#Law 19:18; Kum 6:5Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako. 28#Law 18:5; Mt 19:17Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi. 29Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? 30Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. 31Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando. 32Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. 33#2 Nya 28:15Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 34akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. 35Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. 36Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? 37Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.
Yesu Awatembelea Martha na Mariamu
38 # Yn 11:1; 12:2,3 Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. 39Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. 40Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. 41Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; 42#Mt 6:33lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.

Currently Selected:

Lk 10: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy