YouVersion Logo
Search Icon

2 Nya 1

1
Sulemani Aomba Hekima
1 # 1 Fal 2:46; Mwa 21:22; 39:2; 1 Nya 17:8; 29:25; Mt 28:20 Basi Sulemani, mwana wa Daudi, alithibitishwa katika ufalme wake, naye BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye, akamtukuza mno. 2#1 Nya 27:1; 2 Nya 29:20; 30:2Sulemani akasema na Israeli wote, na maakida wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila shehe wa Israeli wote, wakuu wa nyumba za mababa. 3#1 Fal 3:4Basi Sulemani akaenda mahali pa juu pa Gibeoni, na kusanyiko lote naye; kwani ndipo ilipokuwako hema ya kukutania ya Mungu, aliyoifanya Musa mtumishi wa BWANA jangwani. 4#2 Sam 6:2; 1 Nya 15:1Lakini sanduku la Mungu, Daudi alikuwa amelipandisha kutoka Kiriath-yearimu mpaka mahali Daudi alipolitengenezea; maana amelitandia hema katika Yerusalemu. 5#Kut 27:1; 38:1; 31:2Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanyiza Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya BWANA; Sulemani na kusanyiko wakaiendea. 6#1 Fal 3:4Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
7 # 1 Fal 3:5; Mit 3:5; Isa 58:9 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. 8#1 Nya 28:5Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. 9#1 Fal 3:7Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi. 10#1 Fal 3:9; Zab 119:34,73; Mit 3:13; Yak 1:5; Hes 27:17; Kum 31:2Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi? 11#1 Sam 16:7; 1 Fal 3:11; 8:18Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao; 12#Zab 34:9,10; Mt 6:33; Efe 3:20; 1 Nya 29:25; 2 Nya 9:22; Mhu 2:9basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo. 13Akaja Sulemani kutoka mahali pa juu pa Gibeoni, toka mbele ya hema ya kukutania, mpaka Yerusalemu; akatawala juu ya Israeli.
Shughuli za Jeshi na Biashara za Mfalme Sulemani
14 # 1 Fal 4:26 Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu. 15#1 Fal 10:27; Ayu 22:24Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi. 16Nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi; kila kundi na thamani yake. 17Nao hupandisha, na kuleta kutoka Misri gari kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa mia na hamsini, vivyo watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.

Currently Selected:

2 Nya 1: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy