YouVersion Logo
Search Icon

Obadia Utangulizi

Utangulizi
Jina Obadia lina maana ya “Mtumishi wa Yehova.” Habari za nabii Obadia hazipatikani popote nje ya kitabu hiki. Unabii wa kitabu hiki unahusu hukumu ya Mungu dhidi ya taifa la Edomu, na kukomeshwa na kuangamizwa kwa taifa hilo kwa sababu ya kiburi na udhalimu wake. Waedomu, waliokuwa uzao wa Esau, walijivunia usalama katika ngome zao kwenye Mlima Seiri, kusini mwa Bahari ya Chumvi. Askari wao walitumika katika jeshi la Nebukadneza baada ya Yerusalemu kutekwa na kuteketezwa mnamo 587 K.K. Waedomu waliwadharau watu wa Yuda, na hawakuwasaidia walipopatwa na mikasa ya kuvamiwa na kupigwa na majeshi ya kigeni. Mwanzoni mwa karne ya tisa, Waedomu wenyewe walishiriki zaidi ya mara nne kuiteka Yerusalemu.
Mwandishi
Obadia.
Kusudi
Kudhihirisha hasira kuu ya Mungu na hukumu yake dhidi ya Waedomu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Inadhaniwa kuwa mnamo 605–586 K.K.
Wahusika Wakuu
Waedomu.
Wazo Kuu
Hukumu ya Mungu dhidi ya Waedomu.
Mambo Muhimu
Dharau, kiburi na udhalimu wa Waedomu na hukumu ya Mungu kwao.
Yaliyomo
Maangamizi ya Edomu (1‑14)
Kurejeshwa kwa Israeli (15‑21).

Currently Selected:

Obadia Utangulizi: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in