YouVersion Logo
Search Icon

Maombolezo 3:21-33

Maombolezo 3:21-33 NENO

Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini. Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu. Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu, kwa hiyo nitamngojea.” BWANA ni mwema kwa wale wanaomtumaini, na kwa yule anayemtafuta; ni vyema kungojea kwa utulivu kwa ajili ya wokovu wa BWANA. Ni vyema mtu kuchukua nira bado angali kijana. Na akae peke yake awe kimya, kwa maana BWANA ameiweka juu yake. Hata azike uso wake mavumbini bado tumaini litakuwepo. Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu. Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali na Bwana milele. Ingawa huleta huzuni, ataonesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu. Kwa maana hapendi kuwaletea mateso au huzuni watoto wa wanadamu.

Video for Maombolezo 3:21-33

Verse Images for Maombolezo 3:21-33

Maombolezo 3:21-33 - Hata hivyo najikumbusha neno hili
na kwa hiyo ninalo tumaini.

Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu,
kwa hiyo nitamngojea.”

BWANA ni mwema kwa wale wanaomtumaini,
na kwa yule anayemtafuta;
ni vyema kungojea kwa utulivu
kwa ajili ya wokovu wa BWANA.
Ni vyema mtu kuchukua nira
bado angali kijana.

Na akae peke yake awe kimya,
kwa maana BWANA ameiweka juu yake.
Hata azike uso wake mavumbini
bado tumaini litakuwepo.
Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,
na ajazwe na aibu.

Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali
na Bwana milele.
Ingawa huleta huzuni, ataonesha huruma,
kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.
Kwa maana hapendi kuwaletea mateso
au huzuni watoto wa wanadamu.Maombolezo 3:21-33 - Hata hivyo najikumbusha neno hili
na kwa hiyo ninalo tumaini.

Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu,
kwa hiyo nitamngojea.”

BWANA ni mwema kwa wale wanaomtumaini,
na kwa yule anayemtafuta;
ni vyema kungojea kwa utulivu
kwa ajili ya wokovu wa BWANA.
Ni vyema mtu kuchukua nira
bado angali kijana.

Na akae peke yake awe kimya,
kwa maana BWANA ameiweka juu yake.
Hata azike uso wake mavumbini
bado tumaini litakuwepo.
Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,
na ajazwe na aibu.

Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali
na Bwana milele.
Ingawa huleta huzuni, ataonesha huruma,
kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.
Kwa maana hapendi kuwaletea mateso
au huzuni watoto wa wanadamu.Maombolezo 3:21-33 - Hata hivyo najikumbusha neno hili
na kwa hiyo ninalo tumaini.

Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
Nimeiambia nafsi yangu, “BWANA ni fungu langu,
kwa hiyo nitamngojea.”

BWANA ni mwema kwa wale wanaomtumaini,
na kwa yule anayemtafuta;
ni vyema kungojea kwa utulivu
kwa ajili ya wokovu wa BWANA.
Ni vyema mtu kuchukua nira
bado angali kijana.

Na akae peke yake awe kimya,
kwa maana BWANA ameiweka juu yake.
Hata azike uso wake mavumbini
bado tumaini litakuwepo.
Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,
na ajazwe na aibu.

Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali
na Bwana milele.
Ingawa huleta huzuni, ataonesha huruma,
kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.
Kwa maana hapendi kuwaletea mateso
au huzuni watoto wa wanadamu.

Free Reading Plans and Devotionals related to Maombolezo 3:21-33