YouVersion Logo
Search Icon

Hagai Utangulizi

Utangulizi
Hagai ni moja ya vitabu vitatu vya kinabii vya Agano la Kale vilivyoandikwa baada ya Wayahudi kurudi nyumbani kutoka uhamishoni Babeli. Baada ya Mfalme Dario kutoa amri ya kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu kutoka uhamishoni, Hagai na Zekaria waliwatia moyo watu hao kulijenga upya Hekalu la Bwana.
Kundi la kwanza la Wayahudi liliporudi Yerusalemu liliweka msingi wa Hekalu jipya kwa furaha na matumaini makubwa. Hata hivyo, Wasamaria na majirani wengine walipinga ujenzi huo kwa nguvu nyingi na kuwakatisha tamaa wafanyakazi, na kusababisha ujenzi huo usimame. Watu wakageukia ujenzi wa nyumba zao wenyewe. Nabii Hagai aliwahimiza watu kwamba ulikuwa wakati wa kuanza kujenga upya nyumba ya Mungu.
Mwandishi
Hagai.
Kusudi
Kujenga upya Hekalu la Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 520 K.K.
Wahusika Wakuu
Hagai, Zerubabeli, Yoshua.
Wazo Kuu
Hagai aliwaambia watu kwamba utukufu wa Hekalu walilokuwa wanajenga ungekuwa mkubwa kuliko ule wa Hekalu lililotangulia, ingawaje halingekuwa imara kama la kwanza. Hili Hekalu lingekuwa bora zaidi kwa sababu Mungu angelijaza utukufu wake ndani yake.
Mambo Muhimu
Kuwaita watu kujenga upya Hekalu huko Yerusalemu lililokuwa limebomolewa, na ahadi ya Mungu ya kuwabariki kama wangemtii.
Yaliyomo
Wito wa kujenga Hekalu (1:1‑15)
Matumaini ya Hekalu jipya, na baraka zilizoahidiwa (2:1‑23).

Currently Selected:

Hagai Utangulizi: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in