YouVersion Logo
Search Icon

Habakuki Utangulizi

Utangulizi
Jina “Habakuki” maana yake ni “Kumbatia”. Habakuki alikuwa nabii wa Yuda kutoka kabila la Lawi na alikuwa mmoja wa waimbaji katika Hekalu. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo wa mazungumzo kati ya Mungu na nabii. Habakuki hakuelewa jinsi gani Mungu angeweza kuwatumia Wakaldayo, waliokuwa waovu kuliko Wayahudi, kutekeleza hukumu dhidi ya watu waliokuwa wamechaguliwa na Mungu. Jibu la Mungu lilikuwa kwamba wenye haki wangeishi kwa imani. Mungu alimwambia Habakuki kwamba bila kukawia, Wakaldayo wangehukumiwa na haki ingetawala kwa ajili ya watu wa Mungu.
Mwandishi
Habakuki.
Kusudi
Kuthibitisha kwamba Mungu anatawala dunia na atahukumu kila uovu kwa wakati wake, na kwamba mwenye haki ataishi kwa imani.
Mahali
Yuda.
Tarehe
Mnamo 612–589 K.K.
Wahusika Wakuu
Habakuki, na Wakaldayo.
Wazo Kuu
Mwenye haki ataishi kwa imani.
Mambo Muhimu
Mungu hutumia watu waovu kuwaadhibu watu wake wanapomwasi. Lengo ni kuwarejesha katika uhusiano mwema naye. Hivyo, wenye haki wanapaswa kuishi kwa imani wakijua kuwa Mungu ana mamlaka na haki ya kutumia njia aitakayo kuwaadhibu wakosaji.
Yaliyomo
Swali la Habakuki na jibu la Mungu (1:1‑11)
Swali la pili la Habakuki na jibu la Mungu (1:12–2:20)
Maombi ya Habakuki (3:1‑19).

Currently Selected:

Habakuki Utangulizi: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in