YouVersion Logo
Search Icon

Wakolosai Utangulizi

Utangulizi
Nyaraka za Waefeso na Wakolosai zinaitwa pacha kwa sababu mambo yaliyomo yanafanana. Timotheo alishirikiana na Paulo huko Rumi katika kuandika nyaraka hizi mbili; Wakolosai ni mojawapo ya nyaraka za gerezani. Tikiko ndiye aliupeleka waraka huu Kolosai.
Mji wa Kolosai ulikuwa umejengwa kama kilomita 160 kutoka Efeso kwenye Bonde la Lika, karibu na Hierapoli na Laodikia. Kwa kadiri ionekanavyo, Paulo alikuwa hajautembelea mji wa Kolosai, ila mji huu ulihubiriwa Injili na Epafra wakati Paulo alikuwa Efeso. Paulo alipata kuwafahamu waumini hawa akiwa Efeso katika safari yake ya pili kueneza Injili. Sasa alikuwa na wasiwasi kwa sababu alisikia kuwa mafundisho ya Unostiki yalikuwa yameingia katika kanisa hilo. Mafundisho haya yalikuwa yakiuelekeza ujumbe wa Injili hatarini.
Mwandishi
Mtume Paulo.
Kusudi
Kupinga mafundisho ya uzushi katika kanisa, na kuwaonesha waumini kwamba wana kila kitu wanachokihitaji katika Kristo.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Paulo, Timotheo, Tikiko, Onesimo, Aristarko, Marko, na Epafra.
Wazo Kuu
Kuthibitisha utoshelevu wa Kristo, ukilinganishwa na utupu wa filosofia ya mwanadamu.
Mambo Muhimu
Mambo yaliyokuwa yakiwasumbua Wakolosai: Mchanganyiko wa elimu ya nyota, uchawi, na mafundisho ya Unostiki ambayo yalisema kwamba Kristo alikuwa sawa na malaika.
Yaliyomo
Salamu, shukrani na maombi (1:1‑14)
Yesu Kristo na waumini (1:15–2:7)
Hatari za mafundisho ya uongo (2:8‑23)
Mafundisho kuhusu maisha ya Kikristo (3:1–4:1)
Maagizo zaidi, na mausia ya mwisho (4:2‑18).

Currently Selected:

Wakolosai Utangulizi: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in