1
Waroma 6:23
Swahili Roehl Bible 1937
SRB37
Kwani mshahara wa ukosaji ni kufa; lakini gawio, Mungu analotupa katika Bwana wetu Kristo Yesu, ni uzuma wa kale na kale.
Compare
Explore Waroma 6:23
2
Waroma 6:14
Kwani ukosaji hautashika ufalme, uwatawale, maana nguvu yenu siyo ya Maonyo, ila ya upole.
Explore Waroma 6:14
3
Waroma 6:4
Hivyo tulizikwa pamoja naye tulipobatiziwa, tufe naye, ni kwamba: Kama Kristo alivyofufuliwa katika wafu kwa nguvu ya utukufu wa Baba, vivyo nasi sharti tupate upya wa maisha, tuendelee nao.
Explore Waroma 6:4
4
Waroma 6:13
Wala msivitoe viungo vyenu, viwe mata ya upotovu ya kuyatumikia makosa! Ila mjitoe wenyewe kumtumikia Mungu kwa hivyo, mnavyoishi, tena mlikuwa mmekwisha kufa! Navyo viungo vyenu mvitoe, viwe mata ya wongofu ya kumtumikia Mungu!
Explore Waroma 6:13
5
Waroma 6:6
Kwani tunalitambua neno hili: mtu wetu wa kale amewambwa msalabani pamoja naye, miili yetu yeye kukosa ipate kukomeshwa, sisi tusiyatumikie tena makosa kama watumwa.
Explore Waroma 6:6
6
Waroma 6:11
Nanyi jiwazieni hivyo: makosa mmekwisha kuyafia, lakini sasa mnaishi, mmtumikie Mungu katika Kristo Yesu!*
Explore Waroma 6:11
7
Waroma 6:1-2
Sasa tusemeje? Tufulize kukosa, magawio nayo yafurike? La, sivyo! Sisi tulioyafia makosa tutawezaje kuishi nayo tena?
Explore Waroma 6:1-2
8
Waroma 6:16
Hamjui, vilivyo? Ni hivi: mnapojitoa wenyewe kumtumikia mtu kitumwa na kumtii, basi, mmekwisha kuwa watumwa wake yeye, mnayemtii. Ikiwa ni wa ukosaji, mnakwenda kufa; ikiwa ni wa wito, mnakwenda kupata wongofu.
Explore Waroma 6:16
9
Waroma 6:17-18
Lakini Mungu atolewe shukrani, kwa sababu ninyi mliokuwa watumwa wa ukosaji mmegeuzwa mioyo, mkaja kuyatii mafundisho, kama mlivyoyapata! Napo hapo, mlipokombolewa katika utumwa wa ukosaji, mmegeuka kuwa watumwa wa wongofu.
Explore Waroma 6:17-18
Home
Bible
Plans
Videos