1
Kutoka 16:3-4
BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA
SCLDC10
“Laiti Mwenyezi-Mungu angelituua tulipokuwa nchini Misri ambako tulikaa, tukala nyama na mikate hata tukashiba. Lakini nyinyi mmetuleta huku jangwani kuiua jumuiya hii yote kwa njaa!” Ndipo Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mimi nitawanyeshea mikate kutoka mbinguni. Kila siku watu watatoka na kukusanya chakula cha siku hiyo. Kwa njia hii nitawajaribu nione kama watazifuata sheria zangu au hawatazifuata.
Compare
Explore Kutoka 16:3-4
2
Kutoka 16:2
Basi, jumuiya yote ya Waisraeli ikawalalamikia Mose na Aroni huko jangwani
Explore Kutoka 16:2
3
Kutoka 16:8
Tena Mose akasema, “Jioni, Mwenyezi-Mungu atawapeni nyama mle, na asubuhi atawapeni mikate mle mshibe, maana yeye ameyasikia manunguniko mliyomnungunikia. Sisi ni nani hata mtunungunikie? Msitunungunikie sisi bali mnungunikieni Mwenyezi-Mungu.”
Explore Kutoka 16:8
4
Kutoka 16:12
“Nimeyasikia manunguniko ya Waisraeli. Basi, waambie kwamba wakati wa jioni watakula nyama, na asubuhi watakula mkate. Hapo ndipo mtakapotambua kuwa mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
Explore Kutoka 16:12
Home
Bible
Plans
Videos