Kisha malaika wa tatu akapiga baragumu. Halafu nyota kubwa iliyowaka kama mwenge, ikaanguka toka mbinguni na kujitupa juu ya sehemu moja ya tatu ya mito na juu ya chemichemi. (Jina la ile nyota ni Uchungu.) Basi sehemu moja ya tatu ya maji ikakuwa uchungu, na watu wengi waliokunywa maji yale walikufa kwa sababu ya sumu iliyokuwa ndani yake.