1
Isaya 60:1
BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
SWC02
Simama, ee Sayuni uangaze; maana mwangaza unatokea kwa ajili yako, utukufu wa Yawe unakuangazia.
Compare
Explore Isaya 60:1
2
Isaya 60:3
Mataifa watatembea katika mwangaza wako, wafalme watavutwa na kungaa kwako.
Explore Isaya 60:3
3
Isaya 60:2
Giza litaifunika dunia, giza kubwa litayafunika mataifa; lakini wewe, Yawe atakuangazia, utukufu wake utaonekana kwako.
Explore Isaya 60:2
4
Isaya 60:22
Anayekuwa jamaa ndogo kati yenu atakuwa kabila, anayekuwa mudogo kuliko wote atakuwa taifa kubwa. Mimi ndiye Yawe; wakati utakapofika nitayatimiza haraka.
Explore Isaya 60:22
5
Isaya 60:19
Hautahitaji tena jua kukuangazia muchana, wala mwezi kukuangazia usiku; maana mimi Yawe ni mwangaza wako milele; mimi Mungu wako nitakuwa utukufu wako.
Explore Isaya 60:19
6
Isaya 60:20
Mwangaza wako muchana hautatua kama jua, wala mwangaza wako usiku kufifia kama mbalamwezi; maana Yawe ni mwangaza wako milele, nazo siku zako za kuomboleza zitakoma.
Explore Isaya 60:20
7
Isaya 60:5
Halafu utaona na utafurahi, moyo wako utasisimuka na kushangilia. Maana utajiri tokea ngambo ya bahari utakufikia kwa wingi, mali za mataifa zitaletwa kwako.
Explore Isaya 60:5
8
Isaya 60:4
Inua macho uangalie pande zote; wote wanakusanyika wakuje kwako. Wana wako watafika toka mbali, wabinti zako watabebwa katika mikono.
Explore Isaya 60:4
9
Isaya 60:21
Watu wako wote watakuwa wa haki, nao watarizi inchi milele. Hao ni chipukizi nililopanda mimi, kazi ya mikono yangu kwa ajili ya utukufu wangu.
Explore Isaya 60:21
10
Isaya 60:18
Mateso makali hayatasikilika tena katika inchi yako; wala uharibifu na maangamizi ndani ya mipaka yako. Utaweza kuziita kuta zako: “Wokovu”, na milango yako: “Sifa”.
Explore Isaya 60:18
11
Isaya 60:11
Milango yako itakuwa wazi siku zote; usiku na muchana haitafungwa, kusudi watu wakuletee utajiri wa mataifa, pamoja na wafalme wao katika maandamano.
Explore Isaya 60:11
12
Isaya 60:6
Makundi ya ngamia yataifunika inchi yako, wana wa ngamia kutoka Midiani na Efa; wote watakuja kutoka Seba. Watakuletea zahabu na ubani, wakitangaza sifa za Yawe.
Explore Isaya 60:6
13
Isaya 60:10
Yawe anasema: Wageni watazijenga upya kuta zako, wafalme wao watakutumikia. Maana kwa hasira yangu nilikupiga, lakini kwa wema wangu nimekuhurumia.
Explore Isaya 60:10
14
Isaya 60:15
Wewe ulikuwa umeachwa na kuchukiwa, hakuna aliyependa hata kupita ndani yako. Lakini sasa nitakufanya ukuwe na utukufu milele, utakuwa muji wa furaha kwa kizazi na kizazi.
Explore Isaya 60:15
15
Isaya 60:16
Utaletewa chakula na watu wa mataifa; wafalme watakupatia chakula bora. Hapo utatambua kwamba mimi Yawe ni Mwokozi wako; mimi Mwenye Nguvu wa Yakobo ni Mukombozi wako.
Explore Isaya 60:16