Sasa hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa ufalme wa Israeli
katika siku zile:
nitawawezesha kuchunga sheria zangu ndani ya mafikiri yao,
nikiziandika ndani ya mioyo yao.
Ni Bwana wetu Mungu anayesema hivyo.
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.