1
Luka 8:15
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
TKU
Na zile zilizoangukia katika udongo mzuri, ni wale ambao huyasikia mafundisho ya Mungu kwa moyo safi na mnyoofu. Huyatii na kwa uvumilivu wao huzaa mazao mazuri.
Compare
Explore Luka 8:15
2
Luka 8:14
Zilizoanguka katika miiba, zinafanana na watu wanaoyasikia Mafundisho ya Mungu, lakini wanaruhusu wasiwasi, mali na anasa za maisha haya kuwasimamisha na hawaendelei kukua. Hivyo mafundisho hayazalishi matokeo mazuri katika maisha yao.
Explore Luka 8:14
3
Luka 8:13
Wengine wanafanana na mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye mawe. Ni watu ambao huyasikia mafundisho ya Mungu na kuyapokea kwa furaha, lakini kwa kuwa hawana mizizi yenye kina, huamini kwa muda mfupi. Majaribu yanapokuja, humwacha Mungu.
Explore Luka 8:13
4
Luka 8:25
Ndipo Yesu akawaambia wafuasi wake, “Imani yenu iko wapi?” Lakini wao waliogopa na kustaajabu, wakanong'onezana, “Huyu ni mtu wa namna gani? Anaamuru upepo na maji, na vinamtii?”
Explore Luka 8:25
5
Luka 8:12
Watu wengine ni kama mbegu zilizoanguka njiani. Husikia mafundisho ya Mungu, lakini Shetani huja na kuwafanya waache kuyatafakari. Hii huwafanya kutoamini na kuokoka.
Explore Luka 8:12
6
Luka 8:17
Kila jambo lililofichwa litawekwa wazi na kila siri itajulikana na kila mtu ataiona.
Explore Luka 8:17
7
Luka 8:47-48
Yule mwanamke alipoona ya kwamba hataweza kujificha akajitokeza akitetemeka. Akasujudu mbele ya Yesu. Huku kila mmoja akisikia, akaeleza sababu iliyomfanya amguse, na kwamba alipona wakati ule ule alipomgusa. Yesu alimwambia, “Binti yangu umeponywa kwa sababu uliamini. Nenda kwa amani.”
Explore Luka 8:47-48
8
Luka 8:24
Wafuasi wakamwendea, wakamwamsha, wakasema, “Mkuu, mkuu, tutazama!” Yesu akasimama, akaukemea upepo na mawimbi ya maji. Upepo ukakoma na ziwa likatulia.
Explore Luka 8:24