1
1 Wakorintho 15:58
Swahili Revised Union Version
SRUV
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Compare
Explore 1 Wakorintho 15:58
2
1 Wakorintho 15:57
Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Explore 1 Wakorintho 15:57
3
1 Wakorintho 15:33
Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Explore 1 Wakorintho 15:33
4
1 Wakorintho 15:10
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nilizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
Explore 1 Wakorintho 15:10
5
1 Wakorintho 15:55-56
Kuko wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? Uko wapi, Ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
Explore 1 Wakorintho 15:55-56
6
1 Wakorintho 15:51-52
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
Explore 1 Wakorintho 15:51-52
7
1 Wakorintho 15:21-22
Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
Explore 1 Wakorintho 15:21-22
8
1 Wakorintho 15:53
Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
Explore 1 Wakorintho 15:53
9
1 Wakorintho 15:25-26
Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke adui zake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
Explore 1 Wakorintho 15:25-26
Home
Bible
Plans
Videos