1
Warumi 4:20-21
Neno
NEN
Lakini Abrahamu hakusitasita kwa kutokuamini ahadi ya Mungu, bali alitiwa nguvu katika imani yake na kumpa Mungu utukufu, akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza lile aliloahidi.
Compare
Explore Warumi 4:20-21
2
Warumi 4:17
Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu, ambaye yeye alimwamini, yule Mungu anayefufua waliokufa, na kuvitaja vitu ambavyo haviko kana kwamba viko.
Explore Warumi 4:17
3
Warumi 4:25
Alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu, naye alifufuliwa kutoka mauti ili tuhesabiwe haki.
Explore Warumi 4:25
4
Warumi 4:18
Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Abrahamu akaamini, akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyoahidiwa kwamba, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”
Explore Warumi 4:18
5
Warumi 4:16
Kwa hiyo, ahadi huja kupitia kwa imani, ili iwe ni kwa neema, na ihakikishiwe wazao wote wa Abrahamu, si kwa wale walio wa sheria peke yao, bali pia kwa wale walio wa imani ya Abrahamu. Yeye ndiye baba yetu sisi sote.
Explore Warumi 4:16
6
Warumi 4:7-8
“Wamebarikiwa wale ambao wamesamehewa makosa yao, ambao dhambi zao zimefunikwa. Heri mtu yule Bwana hamhesabii dhambi zake.”
Explore Warumi 4:7-8
7
Warumi 4:3
Kwa maana Maandiko yasemaje? “Abrahamu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki.”
Explore Warumi 4:3