Soma Biblia Kila Siku Mei 2021预览

Kitabu cha Ayubu ni simulizi ndefu ambapo Ayubu alipatwa na mateso mengi. Wakati alipokuwa akiteseka, marafiki zake, Elifazi na wenzake watatu, walimtuhumu Ayubu kwamba alikuwa anapata taabu kwa sababu alikuwa mdhambi. Hawakufahamu kuwa mapito ya Ayubu yalikuwa ni kusudi la Mungu. Ni rahisi kuwahukumu wenzetu kwa jambo lisilo sahihi. Biblia yafundisha: "Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi". Kama una nafasi, tafuta kusoma Mt 7:1-5 kwa ufafanuzi mpana zaidi. Tuwahurumie wenzetu na kuwaombea katika dhiki zao.