Soma Biblia Kila Siku Mei 2021预览

Katika Warumi 1:19 twajifunza kuwa Mungu amedhihirishia wanadamu mambo yake: Mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao [wanadamu], kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Niseme kwa urahisi kwamba Mungu amejidhihirisha kwetu kwa matendo yake makuu. Kila tukionacho duniani ni udhihirisho kwamba yuko Mungu anayehusika na uwepo wa vitu hivyo. Kiboko ni mnyama mkubwa duniani. Kila alichoumbiwa kinatangaza uwepo wa Mungu na uweza wake. Tukumbuke kuwa Mungu alimwumba pamoja nasi – kama anavyomkumbusha Ayubu katika m.15: Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe. Mambo namna hii yatosha kutufanya tumtambue Mungu, kumwamini na kutetemeka mbele zake.