Soma Biblia Kila Siku Mei 2021预览

Ayubu anajuta ujinga wake uliokuwa umefunika ufahamu wake. Huko nyuma alijitetea na kujihesabia haki. Hali ya Ayubu ni kawaida yetu sote. Tunapokuwa hatuyaelewi matendo ya Mungu katika maisha yetu, hususani yaliyo kinyume na matakwa yetu, tunajaribiwa kuona Mungu hawezi, au ametupuuza, au ametuacha. Ukweli ni kuwa yeye huona yote, na katika kila analoruhusu liwe kwetu lina kusudi lake jema. Kwa hiyo tuwe na utayari wa kuomba kufunuliwa makusudi yake na kutubu tunapogundua kupungukiwa kwetu.