Soma Biblia Kila Siku Mei 2021预览

Nyakati nyingi wanadamu hujivuna wakijihesabu kuwa wanao uwezo wa kuamua na kutenda watakacho. Moyo wa namna hii hujawa na kiburi na kujikweza. Nyuma ya pazia la moyo huo ni Ibilisi autawalaye utashi wake. Mungu amtazamapo mtu huyu, humwita mpumbavu kwa kutotambua alivyo maskini na mkiwa. Hana lolote awezalo kutenda. Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu (2 Kor 3:5). Kwa hiyo tumnyenyekee Mungu atuwezesheaye.