Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Tumieni akili, Paulo anawasihi Wakorintho. Kubatizwa kwa ajili ya wafu hakufai kitu, lakini huthibitisha imani katika ufufuo. Jinsi ambavyo Paulo haogopi kufa anapoeneza Injili, inathibitisha vilevile kuwa Kristo amefufuka na ufufuo wake umeshinda vitu vyote. Mbele ya Kristo kifo hakitishi tena. Heri wafu wafao katika Bwana. Ila mazungumzo haya mabaya, "Tule na tunywe, maana kesho tutakufa" (m.32), huharibu imani na tabia njema. Kwa hiyo Paulo anasihi sana tuishi sawasawa na imani yetu!