Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Paulo anafundisha kuhusu maisha na wajibu wa Mkristo. Wakristo wa Yerusalemu walikabiliwa na njaa na ukame. Mtume akaanzisha utaratibu wa kukusanya fedha ili kuwasaidia. Kumtolea Mungu mapato yetu kunafaa kuratibiwe. Paulo anaelekeza kuwa kila juma kila mkristo atoe mapato yake kwa ajili ya kazi ya Kristo. Ili kuimarisha ushuhuda, mapato ya kanisa yatunzwe na Wakristo wenye sifa njema wanaochaguliwa na usharika wote. Michango ilenge kuwasaidia wahitaji mbalimbali.