Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021预览

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

30天中的第2天

Ijumaa Kuu ni siku ya pekee ya kukumbuka siku aliyokufa Bwana wetu Yesu Kristo. Kuuawa kwake kuliasilisha matukio mbalimbali yanayodhihirisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (ling. ushuhuda wa walinzi katika m.54). Kupasuka kwa pazia la hekalu na makaburi kufumuka kunaonyesha kuondoka kwa matabaka na kuleta haki sawa kwa watu wote mbele ya Mungu. Japo Yesu hakutenda kosa lolote, aliuawa kwa ajili ya dhambi zetu ili kukomboa maisha yetu. Kwa kupigwa kwake tumepona sisi sote tunaomwamini, kama ilivyotabiriwa katika Isa 53:5, Alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More