Soma Biblia Kila Siku 06/2020预览

Nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, ikiwa mioyo yetu inatuhukumu, kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote (m.19-20). Dhamiri yetu inatuhukumu tukijiangalia wenyewe. Hata hivyo Mungu alitupenda kiasi cha Yesu aliutoa uhai wake kwa ajili yetu aki chukua dhambi zetu. Upendo wake ni mkubwa kuliko mioyo yetu (hukumu ya dhamiri yetu). Yeye anafahamu kuamini kwetu na upendo wetu katika mioyo yetu, ingawa sisi ni wenye dhambi. Yeye atatuhakikisha kuhusu kusamehewa dhambi zetu. Amri yake ni kumwamini Yesu (m.23: Hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo).