Soma Biblia Kila Siku 06/2020预览

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

30天中的第5天

Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao (m.10). Hapa Yohana anajumlisha ilivyoandikwa katika m.7-9: Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Kutopenda(m.14) ni tabia ya dunia hii. Angalia neno hili akamwonakatika m.7: Mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwonandugu yake ni mhitaji ...Tusisubiri mpaka ndugu (mhitaji) atakapoomba riziki, lakini tukimwona mhitaji ni wajibu wetu kumsaidia kwa kuwa vitu vyote tulivyopokea tumevipokea kutoka kwake Mungu. Hapa Yohana anakaza kwamba ukweli wetu kwa vyo vyote utaonekana tu (m.18).

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More