Soma Biblia Kila Siku 06/2020预览

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

30天中的第11天

Ushindi wa imani huishinda dunia hii, kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu(m.4). Kuamini kwamba Yesu ni Kristo, yaani Mwana wa Mungu, (Kumbuka: 1 Yoh 4:15 na 2:22), kunashuhudia kuwa mtu amezaliwa na Mungu. Kila akiriye ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu(4:15). Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo?(2:22). Imani ya kweli hutoka katika Neno la Mungu. Mnaamini kwa sababu Neno la Mungu linakaa ndani yenu, Yohana anakumbusha katika 2:14. Imani yetu imeumbwa na Mungu, hutokea kwake. Kwa hiyo si kwa jinsi ninavyojisikia au kama ninavyofikiri. Uhakika unaonyeshwa katika m.2: Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishike amri zake (Neno lake). Bila Yeye hakuna upendo wa kweli.

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More