Soma Biblia Kila Siku 06/2020预览

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

30天中的第1天

Mtume Yohana aliwaandikia Wakristo barua hii wakiwa kama watoto wake katika Mungu (m.18: Watoto, ni wakati …). Mpinga Kristo (m.18) ni mtu anayejiweka katika nafasi ya Kristo. Hujitegemea bila Mungu na bila Mwokozi. Walitoka kwetu (m.19). Wapinga Kristo hawatokei nje ya kanisa, bali wanatokea miongoni mwa washarika. Ni muhimu kuwatambua na kuwapiga vita! Wao ni dalili kwamba siku ya mwisho inakaribia. Pia inaonyesha kwamba tunaweza kuwa washarika bila kweli kumjua Kristo. Katikati ya kundi la Wakristo upo mpakausioonekana kwa macho unaowagawanya waumini na wasioamini katika vikundi viwili. Je, wewe na mimi tuko wapi?

读经计划介绍

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More