Soma Biblia Kila Siku 05/2020预览

Neno kuu la zaburi hii ni: Msifu Mungu wako (m.12)! Tumesikia juu ya mambo mengi makubwa, lakini katika viumbe vyake vyote, anapendezwa zaidi na wale ambao katika unyenyekevu wao hutegemea upendo wake daima. Bwana huwaridhia wao wamchao, na kuzitarajia fadhili zake (m.11). Watu wa Mungu wanatunzwa na kuhifadhiwa kwa mambo yote, lakini zaidi ya hayo Mungu amewapa neno lake ambalo kwa hilo wanaweza kumjua na hivyo kumpendeza zaidi.