Soma Biblia Kila Siku 05/2020预览

Mungu ana nguvu isiyo ya kawaida, na ahadi zake ni za kweli. Kwa njia ya Yesu alitimiza ahadi ya kutuletea Roho Mtakatifu, ambaye ana nguvu, ni mwalimu, tena ni mfariji na mwelekezi. Kutompokea ni sawa na kuwa nje ya matendo makuu ya wokovu wa Mungu. Utii wa imani wa Mitume kwa Yesu ulifanya wampokee Roho Mtakatifu. Ni njia tuliyo nayo sisi pia. Roho Mtakatifu anaingia moyoni mwetu tukimwamini Yesu, na ataendelea kutuongoza tukijinyenyekeza tu kwake na kuwa watii kwa uongozi wake.