Soma Biblia Kila Siku 05/2020预览

Ayubu anataja viini vya mafanikio mbalimbali vipatikanavyo duniani. Huasilika ardhini ambamo sayansi na teknolojia hukifunua kitu kilichostirika (m.11). Hivyo watu wengi hutumaini na kutegemea kuna siku binadamu hukomesha giza (m.3). Hapana shaka maarifa yetu hayajafikia hatua ya kufahamu hasa thamani ya rasilimali hizo. Lakini Ayubu anatukumbusha kuwa ubora na umuhimu wa madini hauongezi hekima machoni pa mtu. Je, unajua hekima inapatikana wapi, na unayo? Kima chake chapita vyote.