Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafuta matokeo ya: Mathayo 6:33

Mathayo 6:33 (BHN)

Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.

Mathayo 6:34 (BHN)

Basi, msiwe na wasiwasi juu ya kesho; kesho inayo yake. Matatizo ya siku moja yanawatosheni kwa siku hiyo.

Mathayo 6:3 (BHN)

Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata mwandani wako asijue ufanyalo.

Mathayo 6:30 (BHN)

Ikiwa basi, Mungu hulivika hivyo jani la shambani ambalo leo liko na kesho latupwa motoni, je, si atawafanyia nyinyi zaidi? Enyi watu wenye imani haba!

Mathayo 6:31 (BHN)

“Basi, msiwe na wasiwasi: ‘Tutakula nini, tutakunywa nini, tutavaa nini!’

Mathayo 6:32 (BHN)

Maana hayo yote yanahangaikiwa na watu wasiomjua Mungu. Baba yenu wa mbinguni anajua kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote.

Mathayo 6:6 (BHN)

Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.

Mathayo 6:9 (BHN)

Basi, hivi ndivyo mnavyopaswa kusali: ‘Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe.

Mathayo 6:10 (BHN)

Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.

Mathayo 6:11 (BHN)

Utupe leo chakula chetu cha kila siku.

Mathayo 6:12 (BHN)

Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea.

Mathayo 6:13 (BHN)

Usitutie katika majaribu, lakini utuokoe na yule Mwovu.’ [ Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]

Mathayo 6:21 (BHN)

Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako.

Mathayo 6:25 (BHN)

“Ndiyo maana nawaambieni, msiwe na wasiwasi juu ya chakula na kinywaji mnavyohitaji ili kuishi, wala juu ya mavazi mnayohitaji kwa ajili ya miili yenu. Je, maisha ni chakula tu au zaidi? Na mwili, je, si zaidi ya mavazi?

Mathayo 6:1 (BHN)

“Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.

Mathayo 6:2 (BHN)

“Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Mathayo 6:4 (BHN)

Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.

Mathayo 6:5 (BHN)

“Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Mathayo 6:7 (BHN)

“Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.

Mathayo 6:8 (BHN)

Msiwe kama wao. Baba yenu anajua mnayoyahitaji hata kabla ya kumwomba.

Mathayo 6:14 (BHN)

“Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi pia.

Mathayo 6:15 (BHN)

Lakini msipowasamehe watu makosa yao, naye Baba yenu hatawasamehe nyinyi makosa yenu.

Mathayo 6:16 (BHN)

“Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate kuonekana na watu kuwa wanafunga. Nawaambieni kweli, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Mathayo 6:17 (BHN)

Wewe lakini unapofunga, paka kichwa chako mafuta, nawa uso wako,

Mathayo 6:18 (BHN)

ili mtu yeyote asijue kwamba unafunga, ila ujulikane tu kwa Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.