Tafuta matokeo ya: Mathayo 6:33
Mathayo 5:34 (BHN)
Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu;
Mathayo 5:35 (BHN)
wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu.
Mathayo 5:36 (BHN)
Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
Mathayo 5:37 (BHN)
Ukisema, ‘Ndiyo’, basi iwe ‘Ndiyo’; ukisema, ‘Siyo’, basi iwe kweli ‘Siyo’. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
Mathayo 5:38 (BHN)
“Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Jicho kwa jicho, jino kwa jino.’
Mathayo 5:39 (BHN)
Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili.
Mathayo 5:40 (BHN)
Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.
Mathayo 5:41 (BHN)
Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili.
Mathayo 5:42 (BHN)
Akuombaye mpe, wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu.
Mathayo 5:43 (BHN)
“Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Mpende jirani yako, na kumchukia adui yako.’
Mathayo 5:45 (BHN)
ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
Mathayo 5:46 (BHN)
Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo!
Mathayo 5:47 (BHN)
Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo.
Mathayo 5:48 (BHN)
Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Mathayo 7:29 (BHN)
Hakuwa kama waalimu wao wa sheria, bali alifundisha kwa mamlaka.
Mathayo 8:1 (BHN)
Yesu aliposhuka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata.
Mathayo 8:2 (BHN)
Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia na kusema, “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!”
Mathayo 8:3 (BHN)
Yesu akanyosha mkono, akamgusa na kusema, “Nataka! Takasika.” Mara huyo mtu akapona ukoma wake.
Mathayo 8:4 (BHN)
Kisha Yesu akamwambia, “Angalia, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani, na kutoa sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Mathayo 8:5 (BHN)
Yesu alipokuwa anaingia mjini Kafarnaumu, jemadari mmoja alimwendea, akamsihi
Mathayo 8:7 (BHN)
Yesu akamwambia, “Nitakuja kumponya.”
Mathayo 8:8 (BHN)
Huyo jemadari akamwambia, “Bwana, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona.
Mathayo 8:9 (BHN)
Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, ‘Nenda!’ Naye huenda; na mwingine, ‘Njoo!’ Naye huja; na mtumishi wangu, ‘Fanya kitu hiki!’ Naye hufanya.”
Mathayo 8:10 (BHN)
Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, “Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli mwenye imani kama hii.
Mathayo 8:11 (BHN)
Basi, nawaambieni kwamba watu wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbinguni.