Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafuta matokeo ya: Mathayo 6:33

Mathayo 20:33 (BHN)

Wakamjibu, “Bwana, tunaomba macho yetu yafumbuliwe.”

Mathayo 21:33 (BHN)

Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda hadi nchi ya mbali.

Mathayo 22:33 (BHN)

Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.

Mathayo 23:33 (BHN)

Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?

Mathayo 24:33 (BHN)

Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo haya yote yakitendeka, jueni kwamba yuko karibu sana.

Mathayo 25:33 (BHN)

Atawaweka kondoo upande wake wa kulia na mbuzi upande wake wa kushoto.

Mathayo 26:33 (BHN)

Petro akamwambia Yesu, “Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakuacha kamwe.”

Mathayo 27:33 (BHN)

Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, mahali pa Fuvu la Kichwa,

1 Mambo ya Nyakati 6:33 (BHN)

Zifuatazo ni koo za wale ambao walitoa huduma hizo: Ukoo wa Kohathi: Hemani, kiongozi wa kundi la kwanza la waimbaji, alikuwa mwana wa Yoeli. Ukoo wake kutokana na Israeli ni kama ifuatavyo: Hemani, mwana wa Yoeli, mwana wa Samueli,

2 Mambo ya Nyakati 6:33 (BHN)

nakusihi umsikie toka huko kwako mbinguni, na umjalie huyo mgeni yote atakayokuomba kusudi watu wote ulimwenguni wapate kujua jina lako na kukutii kama wafanyavyo watu wako Israeli na wapate kufahamu kwamba nyumba hii ambayo nimeijenga inajulikana kwa jina lako.

Yeremia 33:6 (BHN)

“Hata hivyo, mimi nitauponya mji huu na kuwapa watu wake afya; nitawajalia ustawi mwingi na usalama.

Ezekieli 33:6 (BHN)

“Lakini kama yule mlinzi akiona adui wanakuja asipige tarumbeta na watu wakawa hawakuonywa juu ya hatari inayokuja, maadui wakaja na kumuua mtu yeyote miongoni mwao; huyo mtu aliyekufa, atakuwa amekufa kwa kosa lake. Lakini mimi nitamdai mlinzi kifo cha mtu huyo.

Mwanzo 33:6 (BHN)

Kisha wale wajakazi wakakaribia pamoja na watoto wao, wakainama kwa heshima.

Zaburi 33:6 (BHN)

Mbingu ziliumbwa kwa neno la Mwenyezi-Mungu, na vyote vilivyomo kwa pumzi ya mdomo wake.

Isaya 33:6 (BHN)

Enyi watu wa Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama, atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa. Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu.

Hesabu 33:6 (BHN)

Kutoka Sukothi, walipiga kambi yao huko Ethamu, ukingoni mwa jangwa.

Yobu 33:6 (BHN)

Wewe na mimi ni sawa mbele ya Mungu; mimi pia niliumbwa kwa sehemu ya udongo.

Kutoka 33:6 (BHN)

Basi, Waisraeli waliyavua mapambo yao tangu walipoondoka mlimani Horebu.

Mathayo 1:6 (BHN)

naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa Bath-Sheba mke wa Uria).

Mathayo 2:6 (BHN)

‘Ee Bethlehemu nchini Yudea, wewe si mdogo kamwe kati ya miji maarufu ya Yudea; maana kwako atatokea kiongozi atakayewaongoza watu wangu, Israeli.’”

Mathayo 3:6 (BHN)

wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.

Mathayo 4:6 (BHN)

akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: ‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”

Mathayo 5:6 (BHN)

Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Mathayo 7:6 (BHN)

“Msiwape mbwa vitu vitakatifu wasije wakageuka na kuwararua nyinyi; wala msiwatupie nguruwe lulu zenu wasije wakazikanyaga.

Mathayo 8:6 (BHN)

akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza na anaumwa sana.”