Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Tafuta matokeo ya: Mathayo 6:33

Mathayo 6:27 (BHN)

Ni nani miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi sana anaweza kuuongeza muda wa maisha yake?

Mathayo 6:28 (BHN)

“Na kuhusu mavazi, ya nini kuwa na wasiwasi? Tazameni maua ya porini jinsi yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayasokoti.

Mathayo 6:29 (BHN)

Lakini nawaambieni, hata Solomoni mwenyewe na fahari zake zote hakupata kuvikwa vizuri kama ua mojawapo.

Mathayo 6:1 (BHN)

“Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo.

Mathayo 6:2 (BHN)

“Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Mathayo 6:4 (BHN)

Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.

Mathayo 6:5 (BHN)

“Mnaposali, msifanye kama wanafiki. Wao hupenda kusimama na kusali katika masunagogi na katika pembe za njia ili watu wawaone. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao.

Mathayo 6:7 (BHN)

“Mnaposali, msipayuke maneno kama watu wasiomjua Mungu. Wao hudhani kwamba Mungu atawasikiliza ati kwa sababu ya maneno mengi.

Mathayo 6:8 (BHN)

Msiwe kama wao. Baba yenu anajua mnayoyahitaji hata kabla ya kumwomba.

Marko 6:33 (BHN)

Lakini watu wengi waliwaona wakienda, wakawatambua. Hivyo wengi wakatoka katika kila mji, wakakimbilia huko Yesu na wanafunzi wake walikokuwa wanakwenda, wakawatangulia kufika.

Luka 6:33 (BHN)

Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya hayo.

Yohane 6:33 (BHN)

Maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na aupaye ulimwengu uhai.”

Methali 6:33 (BHN)

Atapata majeraha na madharau; fedheha atakayopata haitamtoka.

Waamuzi 6:33 (BHN)

Wamidiani, Waamaleki na watu wote wanaokaa kando ya mto Yordani wakapiga kambi zao katika bonde la Yezreeli.

2 Wafalme 6:33 (BHN)

Kabla hata hajamaliza kusema, mfalme akafika, akasema, “Msiba huu umetoka kwa Mwenyezi-Mungu! Kwa nini niendelee kumngojea tena?”

1 Wafalme 6:33 (BHN)

Hali kadhalika, alitengeneza mlango wa mraba wa kuingia sebuleni. Miimo ya mlango huo ilikuwa ya mizeituni,

Mathayo 10:33 (BHN)

Lakini yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.

Mathayo 13:33 (BHN)

Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga madebe mawili na nusu, hata unga wote ukaumuka.”

Mathayo 14:33 (BHN)

Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, “Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.”

Mathayo 15:33 (BHN)

Wanafunzi wakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?”

Mathayo 18:33 (BHN)

Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?’

Mathayo 20:33 (BHN)

Wakamjibu, “Bwana, tunaomba macho yetu yafumbuliwe.”

Mathayo 21:33 (BHN)

Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda hadi nchi ya mbali.

Mathayo 22:33 (BHN)

Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.

Mathayo 23:33 (BHN)

Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?