Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mazungumzo na MunguMfano

Conversations With God

SIKU 2 YA 14

Mungu anapokuwa tayari kutembea kwenye maisha yetu, ufunuo hudhihirika katika siku-- hata nyakati, na tunaweza kupita sehemu za imani na matendo ambayo hapo awali yalikuwa mageni kwetu. Huu ndiyo ushuhuda wa aina hii ya uamsho wa kiroho maishani mwangu.



Yote yalianza niliposikia kwamba watu wa Mungu wanaitwa kuwa na uhusiano binafsi na Roho Mtakatifu. Nilikuwa nimesoma habari za Roho Mtakatifu katika maandiko, akitenda kazi katika karama zake, nikafurahia uwepo wake, na kuzaa baadhi ya matunda yake lakini sikuwezakumjua. Nilikosaje eneo la uhusiano na Roho katika maisha yangu, sijui. Kwa shauku nilitaka kumjua Roho Mtakatifu kama Mungu kwangu. Yawezekanaje mama wa watoto watatu wadogo kupata muda na nguvu kuzama kwa Mungu bila usumbufu?



Niliishia kutenga sehemu kwenye maegesho ya gari na kuweka dawati, kiti na vitu vya kusoma na kuweka kengele ya kuniamsha saa 10.30 alfajiri., ndiyo 10.30 alfajiri! Nilikuwa na njaa ya kiroho. 



Wakati kengele ilipolia ilikuwa ni muda wa kuamka, na nikajiwekea masharti magumu kwenye akili kuhusu umuhimu wa shauku yangu mpaka niliweza kutupa mashuka. Maegesho hayakuwa zawadi ya juhudi zangu. Pasipo kuepuka, nikajikuta nimejifungia na mbu msumbufu. Macho yangu yalikuwa mazito sikuweza hata kutazama. Nilikuwa nimefika, lakini nini kilifuata? Mtu anamjuaje Roho wa Bwana hatahivyo?  



Kama kawaida nilianza kwa kuimba na kusoma Biblia kwa sauti kwa kuwa hiyo ilikuwa ni njia bora ili kuwa macho, lakini baada ya miezi kadhaa nilipita katika furaha ya nidhamu. Nilijifunza kumtegemea Roho Mtakatifu kufunua mawazo na makusudi ya Baba yangu na kuombea kile alichonifunulia. Maandiko yakawa hai na Roho Mtakatifu akiniongoza. Maombi yakapata ujasiri-- na Bwana alijibu maombi yangu. 

)

Katika hatua za jitihada za mwanzo, nilitaka kujaribiwa kuacha lengo. Lakini nilipotii Roho kwa nguvu, wito wa mara kwa mara kutoka naye na kumjua mimi binafsi, aliweza kunifundisha. Sasa najua kutokana na uzoefu kuwa tuliumbwa kwa ajili ya upendo wa mahusiano wa ndani na Roho Mtakatifu. Anaanzisha maombi yote.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Conversations With God

Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta t...

More

Tunapenda kumshukuru Susan Ekhoff kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.amazon.com/Prayer-That-Must-Power-Conversational/dp/1496185560/ref=sr_1_1?ie=UTF8&qid=1498693709&sr=8-1&keywords=prayer+that+must+the+power+of+conversational+prayer

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha