Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 09/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

SIKU 11 YA 30

Kusudi la Mungu kwa maisha ya watakatifu, yaani watu waliokubali kumwamini na kufuata Yesu Kristo, ni kufarijiana na kutiana moyo. Tena yajae ushuhuda juu ya msamaha wa Mungu. Kusameheana kunakojenga na kufariji kunaasilika katika msamaha unaopatikana kwa Yesu Kristo. Hakuna dhambi ambayo haisameheki kama ikitubiwambele za Kristo(m.10). Msamaha huu huwahusu watu wote, si wanakanisa tu. Kutoa na kupokea msamaha iwe ni tendo la daima. Katika Mt 6:12 Yesu anatufundisha kuomba hivi:Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Ukikumbuka ombi hivi, tafakari m.5-11:Iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote. Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi; hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi. Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu. Maana naliandika kwa sababu hii pia, ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote. Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo, Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2025

Soma Biblia Kila Siku 09/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha 1 Nyakati na 2 Wakorintho. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz

Mipangilio yanayo husiana