Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2025Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2025

SIKU 1 YA 31

Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia(m.2). Ufunuo huu bila shaka ulitolewa na mmoja wa manabii wao. Wakati Sauli alipookoka Yesu alimjulisha kwamba atafanya kazi ya misioni. Yesu alimwambia Anania amsaidie Sauli kwa sababu huyu nichombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli(Mdo 9:15). Miaka iliyofuata Mungu alikuwa anamwandaa kwa kazi hii. Sasa muda wake ulikuwa umefika, na kanisa lilithibitisha wito wake na kumtuma. Mtu binafsi kupewa wito pamoja na uongozi wa kanisa kutoa wito ni vitu viwili vinavyokwenda pamoja kwa uongozi waRoho Mtakatifu(m.4)!

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2025

Soma Biblia Kila Siku 05/2025 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi Mei pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.somabiblia.or.tz