Kuua Nguvu zinazoangamiza na John BevereMfano

Leo nitakuonyesha uongo uliojificha ambao unaowaongoza Wakristo katika ibada ya sanamu—hata wakati huu.
Kufanya hivyo, ninataka ufikirie kuhusu hadithi ya ndama wa dhahabu katika Mlima Sinai. Ikiwa unakumbuka, Mungu alikuwa ameokoa wana Waisraeli kutoka Misri kupitia miujiza mingi ya nguvu na kuwaongoza nyikani hadi Mlima Sinai. Alinena amri zake kwao, lakini wote waliogopa na kusisitiza kwamba Musa apande mlimani kuzungumza na Mungu peke yake.
Musa anapoondoka, watu wakakosa subira. Wanamwendea kaka yake Musa, Haruni, na kudai kwamba awatengenezee miungu kuwaongoza kwenye Nchi ya Ahadi. Sasa, neno walilotumia la “miungu” ni Elohim, ambalo linatumiwa katika Agano la Kale kumaanisha miungu wa pagani na Mungu wa kweli, kwa hivyo bado hatujui kwa uhakika ni nani ambaye wanamzungumzia.
Haruni anasalimu amri kwa maombi yao, anatengeneza sanamu ya ndama wa dhahabu, na wanasema, “Ee Israeli, huyu ndiye mungu wenu aliyewatoa nchi ya Misri” (Kutoka 32:4). Bado hatujui wanaongelelea Mungu gani, lakini Haruni anaiweka wazi mara moja.
Anasema, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa ajili ya Bwana” (Kutoka 32:5). Panapoandikwa, “Bwana,” kilichoandikwa ni jina, “Yahweh,” yaani jina la Mungu. Sasa tunajua ni nani wanamzungumzia.
Haya ndiyo mambo yanayoendelea: Wanatangaza, “Yahweh ni Mungu wetu. Yahweh alituokoa kutoka Misri. Yahweh ni Bwana wetu,” ilhali wanaabudu sanamu. Lazima tuione hii kama onyo, kwa sababu ikiwa waliweza kuwa na matangazo sahihi ilhali waliendelea kuabudu sanamu, tunaweza kufanya hivyo pia.
Kwa hakika, Wakristo wengi wanafanya hivi kila siku. Wanatangaza, “Yesu ni Bwana,” lakini hawamfuati Yesu. Kama vile Israeli walisema kwamba waliabudu Yahweh, lakini wakafuata tamaa zao badala ya matakwa yake Mungu ambayo aliyoyatamka, Wakristo wengi wanateua na kuchagua vifungu vya Maandiko ambavyo wanataka kufuata, na kupuuza yale mengine yanayowatatiza!
Huu ni kuunda nakala ya Yesu—sanamu. Hii si kumwabudu Yesu kwa kweli.
Swali ambao tunafaa kuuliza ni, tutajuaje kwamba tunaabudu Yesu wa kweli, wala si nakala ya Yesu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Kama Superman, ambaye anaweza kushinda kila adui, wewe kama mfuasi wa Kristo una uwezo wa kimiujiza kushinda changamoto unazopitia. Lakini shida yako na shida ya Superman ni kwamba nguvu zinazokudhoofisha zipo. Mpango huu utakusaidia kung'oa nguvu hizo maishani mwako, ili uweze kutimiza uwezo ambao Mungu alikupa na kuukumbatia maisha mwako bila mipaka.
More