Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

SIKU 1 YA 31

Yohana Mbatizaji ni nabii wa mwisho wa Agano la Kale, tena ni mkuu kuliko manabii wengine, kwa sababu amepewa wajibu wa pekee wa kumtengenezea Bwana mwenyewe njia. Kazi ya Yohana ilileta uamsho mkubwa kwa Wayahudi, watu walimjia kwa wingi, kama ilivyoelezwa katika m.12:Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. Lakini pamoja na Yesu yanaanza majira mapya ambayo ni kutimizwa kwa maneno yote ya manabii. Ni majira ya ufalme wa Mungu kukaribia kwetu.Aliye mdogo katika ufalme wa Mungu, maana yake ni mwanafunzi wa Yesu. Ndivyo anavyoeleza wazi katika Mt 10:42:Mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, .... Yesu anamaanisha kuwa wanafunzi wake ni wakubwa kuliko Yohana.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2024

Soma Biblia Kila Siku 05/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa tano pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Ku...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha