Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Wimbo Wa NeemaMfano

Wimbo Wa Neema

SIKU 1 YA 5

"Je, mtu yeyote anawezaje kunipenda?"

Umewahi kufikiria kitu kama hicho? Mimi nimewahi.

Nikikua, sikuwa mkamilifu. Hata sasa bado mimi sio mkamilifu. Lakini kama kijana, nilikuwa na hatia na aibu nyingi sana. Watu wangeniambia, " Mungu anakupenda," au " Mungu ana mipango mizuri na maisha yako." Lakini ni vigumu sana kuamini kitu hicho unapojihisi hufai... usiyependwa kabisa.

Ndio maana napenda hadithi ya wimbo wa "Neema ya Ajabu."

Katika neema ya Yesu,

Nimeokolewa,

Nilipotea dhambini,

Nilikuwa kipofu rohoni.

Iwapo umewahi kwenda kanisani au la, unaweza kuwa unajua wimbo huu. Wimbo uliorekodiwa sana katika historia, "Neema ya Ajabu" umeimbwa na Elvis, Aretha Franklin, na Bono. Uliimbwa wakati Nelson Mandela alipochukua hatamu ya uongozi na hata ukawekwa kwenye Simpons!

Lakini usichokijua ni kwamba wimbo wa "Neema ya Ajabu" uliandikwa na nahodha wa meli ya watumwa, John Newton karne ya kumi na nane.

Newton alikuwa na sifa ambayo ingefanya wengi wetu wajione safi wakijilinganisha naye. Unadhani umefanya makosa? Unadhani wewe ni mchafu? Newton alikuwa na hatia ya kuuza watu ili kupata mapato.

Kwa hivyo mtu huyu angeandikaje wimbo akifurahia jinsi Mungu alivyompenda?

Jibu ni neema.

Habari njema ya Yesu Kristo sio ile ambayo mimi na wewe tunaweza kutosha kujiosha nayo ili tupendwe na Mungu.Ni kwamba, tunapojua mabaya yetu, bado Mungu alikuja kwetu kwa upendo ili kutuokoa na dhambi zetu.

Warumi 5: 8 inasema, " Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi; kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali kwenye dhambi. (NIV)

John Newton aliishi miaka mingi akidhihaki neema ya Mungu. Alikuwa amesikia kuhusu upendo wa Mungu kama nilivyosikia nikikua. Yawezekana umeyasikia mambo haya pia. Lakini hakuyaamini…hakutaka kuyaamini.

Usiku mmoja akiendesha meli yake kwenye dhoruba kali, alimlilia Mungu amrehemu. Meli yake ilipopita katika dhoruba salama, aliweka imani yake kwa Yesu mwishowe na akapokea neema ambayo alikuwa ameikataa kwa muda mrefu.

Baadaye, Newton alichangia katika kumaliza biashara ya watumwa Uingereza. Akawa mhubiri, akawatunza maskini, akajengea sifa kama mchungaji ambaye aliwaleta watu kutoka jamii mbalimbali pamoja.

Neema ya Mungu haikumwokoa tu Newton, ilimbadilisha pia.

Lakini haijalishi Newton alivyokua katika uhusiano wake na Mungu, kamwe hakusahau kwamba yote haya yalikuwa kwa neema. Dhambi yake ilistahili hukumu. Dhambi zetu pia zinastahili. Lakini upendo wa Mungu ulimwongoza kumimina hukumu hiyo kwa Yesu, ambaye kwa hiari alichukua mahali petu msalabani. Hii ni neema ya kushangaza.

Baadaye, Newton alisema katika maisha…

"Nakumbuka mambo mawili: kwamba mimi ni mtenda dhambi - na kwamba Kristo ni Mwokozi mkubwa!"

Kwa hivyo, vipi kuhusu hatia na aibu? Vipi kuhusu makosa yako? Vipi kuhusu yale mambo uliyoyafanya au uliyoyasema ambayo unatamani ungeyabadili? Je, hupendwi? Je, dhambi zako ni nyingi sana kuliko neema ya Mungu?

Tujifunze kutoka kwa Newton leo na tujiweke katika ukweli mkubwa kwamba upendo wa Mungu hautegemei thamani yetu, na neema yake ni ya kutosha kabisa kuokoa mtu mwenye dhambi kama mimi.

Baraka,

--Nick Hall

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Wimbo Wa Neema

Gundua undani wa upendo wa Mungu kwako kupitia ibada hii ya Wimbo wa Neema. Mwinjilisti Nick Hall atakuongoza kupitia ibada yenye nguvu ya siku 5 akikualika kujiunga na Wimbo wa neema ya Mungu unaoimbwa juu yako.

Tungependa kuwashukuru PULSE Outreach kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://anthemofgrace.com/

Mipangilio yanayo husiana

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha