Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

SIKU 8 YA 31

Baadhi ya wanafunzi wa Yesu hawakumwamini, kwa kuwa walimwelewakimwilialiposema ndiye chakula kilichoshuka kutoka mbinguni ili wale. Waliona ni neno gumu na wakamwacha Yesu. Je, neno hili ni gumu pia kwako? Au unajibu kama Petro? Zingatia kuwa mwili haufai kitu. Kumwamini Yesu ni zawadi yenye neema toka kwa Mungu kwa njia ya Roho wake ambaye anakaa ndani ya maneno ya Yesu. Bwana Yesu alisema,Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima(m.63). Mwombe Mungu akujalie! Halafu msikilize Yesu, maana hakuna mwingine yeyote mwenye maneno ya uzima. Useme kama Petro,Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele(m.68).

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithal...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha