Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Mei 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Mei 2023

SIKU 1 YA 32

Maana ya m.1 inaonekana vizuri zaidi katika Biblia ya Habari Njema: Sasa, kwa vile tumefanywa kuwa waadilifu kwa imani, basi tunayo amani naye Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Ndugu msomaji, naomba habari hii njema uipokee ipate kukufariji! Kushinda kwako katika hukumu ya Mungu siku ya mwisho kunategemea Yesu Kristo peke yake wala hakutegemei tendo lo lote kwako. Huna sababu ya kuhofu ukimwamini Yesu, maana amani na Mungu umepata bure kwa neema kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu (m.2). Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake (m.9-10).

Andiko

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Mei 2023

Soma Biblia Kila Siku/Mei 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/