Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

SIKU 4 YA 30

Uliyebatizwa na kumkubali Yesu kuwa Mwokozi wako, jua hakika kuwa Yesu Kristo anakuombea kwa Mungu Baba Mbinguni! Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea (Rum 8:34). Hutuombea nini? Somo la leo latupa jibu. Anatuombea ulinzi. Tutalindwa kwa kuliitia jina la Yesu Kristo. Mungu atulinde na nini? Atulinde na mafarakano. Yaani, Wakristo tuwe na umoja (m.11,Kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo). Pili atulinde na yule mwovu, yaani Shetani (m.15, Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu). Halafu anatuombea utakaso. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli (m.17).

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023

Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kat...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha